Salamu – Aprili, 2023

Bwana Yesu Kristo asifiwe mpendwa. Namshukuru Mungu sana aliyetupa uzima na afya kiroho na kimwili. Mwezi huu wa tano tunatarajia kuwa na semina za safari ndefu sana.

Mwezi wa tano ndipo tunapoanza semina za hema viwanjani. mwezi huu tunaanzia kwanza na semina ya wanawake, na tutakua huko Chimala Tarehe 12-14/5/2023, semina hii tunaiandaa sisi wenyewe katika huduma ya Husonemu. Tutafanyi katika kanisa la Lutherani.

Paada ya semina hiyo tutaanzia mkoa wa Kigoma, tutakuja, Katavi pale Mpanda, tutakuja Rukwa pale Sumbawanga mjini, tukitokea hapo tutakuwa Songwe Pale Tunduma. na Tutakwenda tena Chimala katika hema.

Safari hiyo inaanzia mwezi wa tano mpaka mwezi wa saba. mfululizo mwezi wa nane tutapumzika kidogo na mwezi wa tisa tunaanza safari ndefu. Ukiingia katika tovuti yetu utaiona ratiba yetu.

Hebu tuanze kupokea salamu za mwezi wa saba. Kumbuka tuna somo lenye kichwa WEKA BIDII YA KUUSHUGHULIKIA MOYO AU NAFSI YAKO

Kumbuka tunaendelea kujifunza eneo lile la madhara ya kuihifadhi uchungu moyoni mwako.

Mwezi huu tuliangalie jambo la nane lingine.

8: UTAKUA MTU WA KULAUMU WATU NA KUHUKUMU WENGINE NA NAKUJITETEA

Angalia mistari hii “Naliamini, kwa maana nitasema, Mimi naliteswa sana. Mimi nalisema kwa haraka yangu, Wanadamu wote ni waongo.” (Zaburi 116:10-11). Ukiisoma mistari hiyo unaona Daudi alipitia kwenye mateso. mateso hayo yalimuumiza moyoni na anasema wazi kuwa aliteswa sana.

Mateso yale yalimtengenezea kuwa na tabia ya kuhukumu. angalia hapo Daudi anasema alipoteswa na waliomtengenezea hao watu mfumo wa mateso ni wanadamu. aliona kila mwanadamu aliye duniani ni mwongo.

Ukiipitia hiyo mistari utaona uchungu huo ulimtengenezea Daudi tabia ya kuhukumu na kujitetea.

Daudi anadai watu wote ni waongo, je! Ni kweli kila mwanadamu ni mwongo? Tena ukiisoma hiyo mistari unajifunza kuwa chanzo cha mateso ya Daudi ni mwanadamu. Swali la kujiuliza hivi kila mwanadamu alimtengenezea Daudi mateso?

Ni kweli kabisa kwa macho ya kibinadamu unaona wanadamu ndiye wanaye watengenezea watu mateso, kwa kweli kwa namna tunavyoona chanzo cha mateso ya watu ni wanadamu. Lakini ukiisoma Biblia utajifunza chanzo cha mateso ya watu ni shetani. shetani huwatumia wanadamu ili awatumie hao wanadamu kuwatesa watu.

Kama ni mtu anayehukumu kwa haki atagundua kuwa shetani ndiye chanzo cha mateso kwa watu. Ukilijua hili huwezi kumuhukumu mtu. Utamuhukumu shetani. Sasa angalia mtu anapokutana na mateso huwa na tabia ya kuwahukumu watu kwa haraka.

Uchungu wa moyoni huwa unatabia ya kuhukumu watu. Na kuhukumu ni dhambi. ebu ondoa tabia ya kumuhukumu mtu na kujitetea. Ukiona unatabia ya namna hiyo ya kuhukumu, kulaumu watu nk TUBU. GEUKA. ACHANA NA TABIA HIYO. Mwambie Mungu akuondolee uchungu moyoni mwako.

Namini umenielewa Mungu akubariki sana tuonane tena mwezi ujao katika kona hii. .

Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo:-

 1. App yetu ya huduma yenye jina “MWAKATWILA (HUSONEMU)” utaipata Play Store ambapo kuna masomo mengi sana hapo.
 2. Tovuti yetu ya www. mwakatwila. org
 3. YouTube – Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
 4. Facebook ingia katika hiyo tovuti (website) yetu utaona alama ya Facebook (f) “like” na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
 5. Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”
 6. DVDs au CDs
 7. VITABU. Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata VITABU, DVD & CD.
 8. Kwa njia ya REDIO: – Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
 • Rungwe FM 102. 5 Kila siku ya Jumapili saa tatu mpaka saa nne usiku.
 • Baraka FM 107. 7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
 • Bomba FM 104. 1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.

Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:- radio. mwakatwila. org

Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:- +255 754 849 924 au +255 756 715 222

Wako: Mwl Mr & Mrs Steven Mwakatwila.