Salamu – Machi, 2023

Bwana Yesu Kristo asifiwe mpendwa. Namshukuru Mungu atupaye uzima. Nimekuletea salamu za mwezi wa tatu. Karibu uzipokee.

Kumbuka tuna somo lenye kichwa WEKA BIDII YA KUUSHUGHULIKIA MOYO AU NAFSI YAKO

Kumbuka tunaendelea kujifunza eneo lile la madhara ya kuihifadhi uchungu moyoni mwako. Hebu tuliangalie jambo lingine.

7: MTU ALIYE NA UCHUNGU MOYONI HAPOKEI JAMBO JIPYA AU KULIFANYA JAMBO JIPYA LA MAFANIKIO

Watu wengi walioumizwa moyoni na kuhifadhi uchungu hawawezi kulipokea jambo lililo jipya.

Sikia, ili ulipokee jambo jipya au Mungu akupe jambo jipya nilazima ukubali kuyasahau yale mabaya uliyoyafanya au uliyofanyiwa na kukutengenezea uchungu au huzuni.

Biblia inasema “Msiyakumbuke mambo ya kwanza, wala msiyatafakari mambo ya zamani. Tazama, nitatenda neno jipya; sasa litachipuka; je! Hamtalijua sasa? Nitafanya njia hata jangwani, na mito ya maji nyikani. ” (Isaya 43:18-19). Kwa mujibu wa mistari hiyo unaona kuwa ili upewe jambo jipya lazima usiyakumbuke mambo ya kwanza.

Sikia; mtu mwenye uchungu hujikuta akiyatafakari sana mambo aliyofanyiwa na mtu nk. Unajua ni rahisi sana ukajikuta ukiyatafakari mambo magumu uliyoyabeba moyoni.

Kwa mujibu wa maneno hayo ha Mungu utaona shida inayosababisha watu wasipokee jambo jipya ambalo Mungu amepanga kuwapa ni hili la kutokulisahau jambo la zamani. fahamu Mtu wa namna hiyo ni ngumu sana kupokea jambo jipya. Lile jambo la uchungu ulilolihifadhi moyoi fahamu ndiyo kiziuzi cha jambo jipya ambalo Mungu anataka kukupa.

Mfano mtu mwenye uchungu moyoni hawezi waza jambo lolote. mpaka atakapoamua kuliacha wazo la uchungu aliloliwekea moyoni. Ili ufanikiwe kupewa vitu vipya na Mungu anza leo kuyasahau mambo ya zamani, ondoa kufikiria aliyekudhurumu, aliyekuibia nk.

Kama umeondolewa kazini acha kufikiria jambo hilo na kuwa maswali mengi ukijiuliza kwanini umefukuzwa kazi, ondoa kuwaz awee kujiuliza kwanini amenifanyia hivyo. Weka maamuzi ya kutokukumbuka mambo ya zamani yanayokukufanya uyatafakari. . ndipo Mungu atakupa kitu kipya.

Namini umenielewa Mungu akubariki sana tuonane tena mwezi ujao katika kona hii. .

Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo:-

 1. App yetu ya huduma yenye jina “MWAKATWILA (HUSONEMU)” utaipata Play Store ambapo kuna masomo mengi sana hapo.
 2. Tovuti yetu ya www. mwakatwila. org
 3. YouTube – Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
 4. Facebook ingia katika hiyo tovuti (website) yetu utaona alama ya Facebook (f) “like” na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
 5. Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”
 6. DVDs au CDs
 7. VITABU. Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata VITABU, DVD & CD.
 8. Kwa njia ya REDIO: – Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
 • Rungwe FM 102. 5 Kila siku ya Jumapili saa tatu mpaka saa nne usiku.
 • Baraka FM 107. 7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
 • Bomba FM 104. 1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.

Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:- radio.mwakatwila.org

Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:- +255 754 849 924 au +255 756 715 222

Wako: Mwl Mr & Mrs Steven Mwakatwila.