Salamu – Februali, 2023

Bwana Yesu Kristo asifiwe mpendwa.. mimi na familia yangu tunamshukuru Mungu aliyetupa mwezi huu wa pili.

Mwezi uliopita tumekuwa na semina Katika kanisa la Moravian Iyunga jijini Mbeya. Tulikuwa na semina nzuri sana. Tulimuona Mungu alituhudumia vizuri sana

Hebu tuanze kupokea salamu za mwezi huu wa pili fahamu Tunaendelea na salamu zenye kichwa

WEKA BIDII YA KUUSHUGHULIKIA MOYO AU NAFSI YAKO

Hebu tuangalie jambo la sita  ambalo linatengeneza madhara kwa mtu aliyeifadhi huzuni au uchungu moyoni mwake. Nalo ni hili.

  1. HASIRA KALI NA UCHUNGU MOYONI HUWA MTU WA KELELE

Sikia jambo lingine ambalo linanaweza kumbana mtu mwenye uchungu moyoni ni hili la kumtengenezea mtu wa namna hiyo  kuwa na tabia ya kuongea kwa kelele

Biblia inasema hivi “Watu huugua toka mji ulio na watu wengi, Na roho yake aliyejeruhiwa hupiga ukelele; Wala Mungu hauangalii upumbavu.“(Ayubu 24:12)

Mtu aliyejeruhiwa moyoni huwa na tabia ya kupiga makelele.. mtu wa namna hii huongea kwa ukali na kelele.

Mtu wa namna hii kiukweli huwa na shida ya kuwakimbiza watu waliojilani na wewe, Biblia husema mtu wa namna hii huwa na tabia ya upumbavu. Mtu wa namna hiyo husema maneno yaliyojaa ukali na makelele mimi naita magomvi ya kinywa.

Biblia inasema wazi kuwa mtu wa uchungu moyoni hubeba kelele kinywani mwake.. Angalia mistari hii.. “Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya;”( Waefeso 4:31)

Kwa mujibu wa mistari hiyo unaona kuwa mtu mwenye tabia ya uchungu moyoni huwa nimtu mwenye ghadhabu na kelele. Mtu wa namna hii hujikuta ni mtu wa matukano yaani maneno ya kipumbavu.

Jifunze mpendwa kutokuwa na tabia hii ya kuuhifadhi uchungu moyoni,utajikuta ukiwa na tabia mbaya ya kelele. Mungu hapendi tuwe watu wenye ukali wenye kelele.

Nakushauri tubu,anza kujirekebisha ondoa kukarisha uchungu humo moyoni mwako.Ndipo utakuwa ni mtu mwenye kinywa kilicho jaa baraka na neema.

Namini umenielewa Mungu akubariki sana tuonane tena mwezi ujao katika kona hii….

Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo:-

  1. App yetu ya huduma yenye jina “MWAKATWILA (HUSONEMU)” utaipata Play Store ambapo kuna masomo mengi sana hapo.
  2. Tovuti yetu ya www.mwakatwila.org
  3. YouTube – Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
  4. Facebook ingia katika hiyo tovuti (website) yetu utaona alama ya Facebook (f) “like” na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
  5. Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”
  6. DVDs au CDs
  7. VITABU. Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata VITABU, DVD & CD.
  8. Kwa njia ya REDIO: – Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
    • Rungwe FM 102.5 Kila siku ya Jumapili  saa tatu mpaka saa nne usiku.
    • Baraka FM 107.7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
    • Bomba FM 104.1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.
  9. Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:-  radio.mwakatwila.org

Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:-

+255 754 849 924 au +255 756 715 222

Wako

Mwl Mr & Mrs Steven Mwakatwila.