Salamu – Januari, 2023

BwanaYesu Kristo asifiwe mpendwa.. Hongera na mwaka mpya.. Ni jambo la kumshukuru Mungu mnoo kwa kutupatia mwaka huu wa 2023

Naamini Mwaka huu kuna mambo mema Mungu amekuandalia. Jipange naye vizuri tu.

Mwezi ulipoita tumekua na semina mbili..tumekuwa na semina Moraviani Nzovwe jijini Mbeya na tumekua na kambi ya maombi..

Kambi hiyo ilikua nzuri sana… Mwaka huu tunatarajia kuwa nakambi hiyo tena..litakuwa kambi letu la kumi na nne. Karibuni sana..tutaanza tarehe 28-31/12/2023..

Panga kuja Jijini Mbeya katika hilo kambi tutakua pale St Marys Karibuni na ombea kambi hii…

Mwaka tunatarajia kuwa na semina nyingi mnoo..tuombee pia usisite kutoa sadaka yako kwa ajili ya kugharamia semina hizo..unaweza tuma sadaka zako kwa namba 0754849924..

Ukifuatilia katika tovuti yetu utaona Acc yetu ya benki na maelezo mengine..

Hebu tuanze kupokea salamu za mwezi huu wa kwanza..

Tunaendelea na salamu tulizoanza nazo mwaka jana zenye kichwa

WEKA BIDII YA KUUSHUGHULIKIA MOYO AU NAFSI YAKO

Ebu tuangalie jambo la tano ambalo linatengeneza madhara kwa mtu aliyeifadhi huzuni au uchungu moyoni mwake. Nalo ni hili.

5: HUZUNI HUONDOA NGUVU ZA MUNGU NDANI YA MTU.

Angalia mistari hii uone hiki ninachokuambia “Akamchukua Petro na wale wana wawili wa Zebedayo, akaanza kuhuzunika na kusononeka.Ndipo akawaambia, Roho yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa; kaeni hapa, mkeshe pamoja nami.Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifulifuli, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke; walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe.”(Mathayo 26:37-39) Angalia na mistari hii ”Mwenyewe akajitenga nao kama kiasi cha kutupa jiwe, akapiga magoti akaomba,akisema, Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki; walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke. [Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu. Naye kwa vile alivyokuwa katika dhiki, akazidi sana kuomba; hari yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka nchini.] Alipoondoka katika kuomba kwake, akawajia wanafunzi wake, akawakuta wamelala usingizi kwa huzuni.”(Luka22:41-45).

Kwa mujibu wa mistari hiyo tunajifunza uchungu au huzuni aliyokuwa nayo Bwana Yesu Kristo Ilimuondolea nguvu…

Unaweza kuniuliza ulijuaje ? Angalia majibu aliyoletewa alipokua anaomba ni kutiwa nguvu na malaika kutoka mbinguni.

Kilicho sababisha Bwana Yesu Kristo aishiwe nguvu ni huzuni aliyokuwa nayo moyoni mwake.

Huduma iliyokuwa mbele yake ilihitaji nguvu mnoo…kilichopelekea aishiwe nguvu hizo ni uchungu iliyomjaa moyoni..Akaamua kutafuta msaada wa maombi na yeye mwenyewe kuomba..

Unajua Bwana Yesu Kristo alitafuta wanamaombi wamuombee au washughulikie ile hali ya huzuni iliyokua moyoni mwake.

Sikia aliwaambia wazi kuwa ana huzuni na masononeko moyoni mwake… Akaomba waombe..na Malaika akaja kumtia nguvu..maana yake mbinguni waliona huzuni ile aliyokuwa nayo imempunguzia nguvu akatumwa malaika ili aje amtie nguvu.

Watu wengi wanapokutana na hali hii ya uchungu na huzuni moyoni hawajuikuwa halihiyo huwaondolea nguvu.

Biblia inasema hivi “Naye Nehemia, ndiye aliyekuwa Tirshatha, na Ezra kuhani, mwandishi, na Walawi waliowafundisha watu, wakawaambia watu wote, Siku hii ni takatifu kwa BWANA, Mungu wenu; msiomboleze wala msilie. Maana watu wote walilia, walipoyasikia maneno ya torati.Kisha akawaambia, Enendeni zenu, mle kilichonona, na kunywa kilicho kitamu, tena mpelekeeni sehemu yeye asiyewekewa kitu; maana siku hii ni takatifu kwa BWANA wetu; wala msihuzunike; kwa kuwa furaha ya BWANA ni nguvu zenu.”(Nehemia 8:9-10).

Watu hao walifundishwa kutokulia wala kuuzunika kwasababu walitakiwa wahiifadhi furaha ya Bwana mioyoni mwao ili nguvu za Mungu ziwe na watu hao.

Huzuni huondoa furaha ya Bwana..na furaha ya Bwana ikiondoka watu hao wanakosa nguvu.

Kwahiyo jifunze mpendwa unapoifadhi uchungu au huzuni moyoni mwako kinachotokea kwako ni kuondoka kwa nguvu za Mungu kwako..

Ondoa Huzuni moyoni mwako mpendwa ili nguvu za Mungu zizidi ndani yako.. O,ba Mungu akuhudumie katika kukuondolea huzuni..Tafuta na watu wa kukusaidia kuomba.

Usisite kuwashirikisha shida yako..waalike wakuombee na wewe usiache kuomba

Namini umenielewa Mungu akubariki sana tuonane tena mwezi ujao katika kona hii….

Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo:-

 1. App yetu ya huduma yenye jina “MWAKATWILA (HUSONEMU)” utaipata Play Store ambapo kuna masomo mengi sana hapo.
 2. Tovuti yetu ya www.mwakatwila.org
 3. YouTube – Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
 4. Facebook ingia katika hiyo tovuti (website) yetu utaona alama ya Facebook (f) “like” na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
 5. Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”
 6. DVDs au CDs
 7. VITABU. Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata VITABU, DVD & CD.
 8. Kwa njia ya REDIO: – Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
  • Rungwe FM 102.5 Kila siku ya Jumapili  saa tatu mpaka saa nne usiku.
  • Baraka FM 107.7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
  • Bomba FM 104.1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.
 9. Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:-  radio.mwakatwila.org

Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:-

+255 754 849 924 au +255 756 715 222

Wako

Mwl Mr & Mrs Steven Mwakatwila.