Salamu – Disemba, 2022

Bwana Yesu Kristo asifiwe. Ndugu zangu mimi na familia yangu tunamshukuru Mungu ambaye ametupa nafasi ya kuuona mwezi huu wa kumi na mbili na ni mwezi wa mwisho kwa mwaka huu wa 2022.

Mwezi ulipita tulikua na semina tatu.. Na ni mwezi ambao kwetu tulianza ukurasa mpya wa maisha ya kuishi bila baba mzazi.

Mungu alimtwaa baba yetu Gwasa Antony Mwakatwila. Tukiwa na siku mbili ya semina jijini Mbeya huko Mbalizi baba yetu aliugua ghafra.. Alilazwa katika Hospitali ya rufaa ya kanda jijini Mbeya..

Tulimaliza semina ya siku nane Mbalizi wakati baba hali yake haikua nzuri… Tarehe kumi na nane tulianza semina maalumu kwa ajiri ya wanawake Tukuyu, ilitakiwa tuimalize tarehe ishilini..

Tarehe kumi na tisa baba yetu Mungu alimwita..Tunamshukuru Mungu tulimaliza semina tarehe ishilini na kuludi Mbeya na tarehe ishilini na mbili tukampumzisha jijini Mbeya.

Tunawashukuru mnoo kwa maombi yenu na rambirambi zenu asante sana.

Hebu pokea salamu zetu za mwezi huu wa kumi na mbili. Kumbuka tunasalamu zenye kichwa..

WEKA BIDII YA KUUSHUGHULIKIA MOYO AU NAFSI YAKO

Tuangalie madhara ya nne ambayo utakutana nayo ikiwa utahifadhi uchungu moyoni mwako kwa muda mrefu.

4: MADHARA YA NNE UKIIFADHI UCHUNGU MOYONI UTAJIDHARAU

Sikia ukiifadhi uchungu moyoni mwako kitakachotokea kwako ni kupoteza ile hali ya kujiamini.

Utakua ni mtu uliyejaa fadhaa na ni ngumu kuwa mtumishi mzuri wa Mungu kama usipojifunza kuyaponya majeraha ya moyoni mwako.

Mtu aliyejeruhiwa hajiamini anakua mwangalifu mnoo..anajiangalia kila muda, na hujikakatia tamaa

Uchungu ni miongoni mwa kikwazo kikubwa kwa watumishi wengi na hata hutumika kukuvulugia ile hali ya kujiamini katika kufanya mambo mbalimbali.

Mungu analijua sana jambo hili ndiyo maana ndiyo maana alimwfundisha Yeremia maneno haya..

“ Haya basi, wewe jifunge viuno, ukaondoke ukawaambie maneno yote niliyokuamuru; usifadhaike kwa ajili yao, nisije nikakufadhaisha wewe mbele yao.Maana, tazama, nimekufanya leo kuwa mji wenye boma, na nguzo ya chuma, na kuta za shaba, juu ya nchi yote; juu ya wafalme wa Yuda, na juu ya wakuu wake, na juu ya makuhani wake, na juu ya watu wa nchi hii.“(Yeremia 1:17-18)

Ukisikia kuwa mtukafadhaika fahamu nafsiyake lazimaitakuaimepoteza ujasiri. Mtu aliyebeba huzuni na uchungu lazima atajaa fadhaa tu.. Hawezi kukifikisha kile kakibeba kwa ajili ya huduma au kazi zake tu za kila siku.

Mungu alipokua anampatia Yoshua kazi alimwambia maneno haya…

“ Ikawa baada ya kufa kwake Musa, mtumishi wa BWANA, BWANA akamwambia Yoshua, mwana wa Nuni, mtumishi wa Musa, akasema,Musa mtumishi wangu amekufa; haya basi, ondoka, vuka mto huu wa Yordani; wewe na watu hawa wote, mkaende hata nchi niwapayo wana wa Israeli.Kila mahali zitakapopakanyaga nyayo za miguu yenu, nimewapa ninyi, kama nilivyomwapia Musa.Tangu jangwa hili na mlima huu, Lebanoni, mpaka mto ule mkubwa, mto wa Frati, nchi yote ya Wahiti, tena mpaka bahari ile kubwa upande wa machweo ya jua, hapo ndipo patakapokuwa mpaka wenu.Hapatakuwa mtu ye yote atakayeweza kusimama mbele yako siku zote za maisha yako; kama nilivyokuwa pamoja na Musa, ndivyo nitakavyokuwa pamoja na wewe; sitakupungukia wala sitakuacha. Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana ni wewe utakayewarithisha watu hawa nchi hii niliyowaapia baba zao ya kwamba nitawapa.Uwe hodari tu na ushujaa mwingi, uangalie kutenda sawasawa na sheria yote aliyokuamuru Musa mtumishi wangu; usiiache, kwenda mkono wa kuume, au wa kushoto, upate kufanikiwa sana kila uendako.”(Yoshua 1 1-7)

Mtu wenye jeraha moyoni au mwenye uchungu hawezi kuwa shujaa au hodari. Mtu wa namna hii ni rahisi mnoo kutokufanya kile Mungu kamtuma akifanye.

Jeraha lina sababi huzuni moyoni, au uchungu au umivu furani.. na umivu hilo humtoa huyo mtu kwenye kusudi alilopewa na Mungu

Mtu akihifadhi huzuni ni ngumu mno kutii wito ulioitiwa na Mungu..

mfano Angalia mistari hii utajifunza kitu “ Akamchukua Petro na wale wana wawili wa Zebedayo, akaanza kuhuzunika na kusononeka. Ndipo akawaambia, Roho yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa; kaeni hapa, mkeshe pamoja nami. Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifulifuli, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke; walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe.”(MT 26:37-39).

Bwana Yesu Kristo alijua wito alioitiwa kabisa…..Huzunii ikatengeneza ugumu wa kuutenda wito huo…

Kilichomsaidia Bwana Yesu Kristo ni hiki alilijua ni nini akifanye kuuondoauchungu huo…

Akafanya maamuzi ya kulishughulikia jambo hilo kwa njia ya kuomba .na aliomba msaada wa maombi ili kushughulikia huzuni ya moyoni mwake.

Baada ya kuomba tu..akapata ujasiri na akalifanya lile alilotumwa na Mungu.

Ndugu ebu ondoa uchungu moyoni utaona ghafra haliya kujiamini itakuja kwako na utaanza kuyafanya yale ambayo ulishindwa kuyafanya..

Mungu akusaidie katika hali hiyo..jifunze kuomba msaada kwa Mungu ili akuondolee uchungu huo na fadhaa hiyo uliyonayo.. ondoa hali ya kujihurumia na kutafuta sababu ya kwanini unapitia hayo..jipe moyo songa mbele

Naamini umenielewa Mungu akubariki sana tuonane tena mwezi ujao katika kona hii….

Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo:-

 1. App yetu ya huduma yenye jina “MWAKATWILA (HUSONEMU)” utaipata Play Store ambapo kuna masomo mengi sana hapo.
 2. Tovuti yetu ya www.mwakatwila.org
 3. YouTube – Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
 4. Facebook ingia katika hiyo tovuti (website) yetu utaona alama ya Facebook (f) “like” na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
 5. Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”
 6. DVDs au CDs
 7. VITABU. Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata VITABU, DVD & CD.
 8. Kwa njia ya REDIO: – Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
  • Rungwe FM 102.5 Kila siku ya Jumapili  saa tatu mpaka saa nne usiku.
  • Baraka FM 107.7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
  • Bomba FM 104.1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.
 9. Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:-  radio.mwakatwila.org

Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:-

+255 754 849 924 au +255 756 715 222

Wako

Mwl Mr & Mrs Steven Mwakatwila.