Salamu – Machi, 2024

Bwana Yesu Kristo asifiwe sana. mimi na familia yangu tunamshukuru sana Mungu. Siku zinakimbia huu ni mwezi wa tatu. Naamini umeanza kuuzoea na kuona ni nini cha kufanya kwa mwaka huu.

Mwezi uliopita tumekua na semina nzuri sana hapo Iyunga kwenye kanisa la Moravian tulikua na semina nzuri sana. Mwezi huu wa tatu tutaanza kupokea salamu mpya.

Tutakua na salamu ambazo ndani yake kutakua na mambo ya kiutu uzima, yaani ni masomo ya watu wazima. Naamini tutakapoanza kuzipokea utagundua ni masomo ambayo hatujazoea kuyasikia.

Sasa nataka nikupe kazi ya kufanya. Niombee kwa Mungu ili anipatie neno ambalo utaelewa na utakua kiroho na kiuchumi. Mwombe Roho Mtakatifu ili atufundishe na kutupa kuelewa.

Hebu tuanze kupokea salamu za mwezi wa tatu

JIFUNZE KUTAKA KARAMA AU KUOMBA MUNGU AKUPE KARAMA YA UNABII ILI UPATE KUFANIKIWA KIROHO WEWE NA WATU WENGINE (SEHEMU YA KWANZA)

UTANGULIZI:

Karibu sana ndugu yangu ili tupate kujifunza somo hili..Somo hili ni miongoni mwa masomo ambayo ni adimu sana kuyakuta yakifundishwa. Somo hili ni somo ambalo ndani yake limebeba malengo haya yafuatayo.

MALENGO YA SOMO HILI

  1. Kukutengenezea vema ushirika kati yako na Mungu Ushirika wetu na Mungu umefungwa kwenye neno …Mungu anapotupa somo hili amekusudia kuona unakua na ushirika mzuri na Mungu
  2. Kukusaidia kupewa vema maelekezo au maagizo kutoka kwa Mungu Mungu anatabia ya kutupa maelekezo, ndani ya somo hili tutajua njia ambazo Mungu anazitumia ili kutupa maelekezo. Ili wewe na mimi tufanikiwe ni lazima tujifunze kumsikiliza Mungu anasema nini ili tupate miongozo kutoka kwake katika kila tunachokifanya
  3. Kukuwezesha kusikia sauti na neno la Mungu Unaposoma Biblia unajifunza kuwa. Unaweza kusikiliza neno la Mungu ambalo halijabebwa na sauti ya Mungu.

 

Sikia si kila neno unalolisikia limeletwa na sauti ya Mungu. Biblia inatufundisha kuwa kuna sauti ya Mungu iliyobeba neno lake.

 

Biblia inasema hivi “Wakati huo Samweli akamwambia Sauli, BWANA alinipeleka nikutie mafuta, uwe mfalme wa watu wake Israeli; basi sasa, isikilize sauti na maneno ya BWANA.” (1Samwel 15:1).

Angalia na mistari hii “Mhimidini BWANA, enyi malaika zake, Ninyi mlio hodari, mtendao neno lake, Mkiisikiliza sauti ya neno lake.” (Zaburi 103:20)

Tunaposema kusikia sauti ya neno la Mungu maana yake ni neno la Mungu alilokupa Mungu uliseme au ulitende kwa wakati nk.

Sikia unaweza kusikiliza neno la Mungu ambalo huyo anayelisema hakupewa na Mungu aliseme au alihubiri. Ni yeye tu kalipenda analielewa sana kaamua kulihubiri au kulifundisha.

Mtu wa namna hiyo hulisema neno la Mungu lililobeba sauti ya huyo aliyelisema. Watu wengi sana hatuna muda wa kumuuliza Mungu ni neno gani ambalo umepanga kulihubiri au kulifundisha mahali hapo.

Wengi hulisema neno la Mungu lakini ukimuuliza Mungu anaweza kukuambia si yeye amekutuma ulihubiri au ulifundishe neno hilo.

Umewahi jiuliza swali kwanini watu wengi wanasikia sana neno la Mungu lakini hawabadiliki? Jibu moja wapo ni hili hili angalia mistari hii “Lakini kama wangalisimama katika baraza yangu, ndipo wangaliwasikizisha watu wangu maneno yangu, na kuwageuza waziache njia zao mbaya, na uovu wa matendo yao.23 Mimi ni Mungu aliye karibu, asema BWANA, mimi si Mungu aliye mbali.” (Yeremia 23:22-23)

Kwa mujibu wa mistari hii utajifunza kuwa ni rahisi sana ukatoka na neno la Mungu ambalo chanzo chake kimetoka kwa mtu. Ngoja nikupe mfano, hujawahi sikia mtu anahubiri au fundisho somo ambalo chanzo chake ni mchungaji au askofu kamwambia hubiri somo furani? Na mtu huyo anenda kutafuta mistari inayofanana na agizo la askofu au mtumishi.

Sikia, ukiona mtu anahubiri au anafundisha somo la namna hiyo mara nyingi mtu huyo anayehubiri hivyo ana toa sauti ya aliyemtuma .

Sikia ndani ya somo hili tutajifunza kupokea neno la Mungu lililo ambatana na sauti yake.

 

  1. Kukupatia maarifa,hekima,na ufahamu kutoka kwa Mungu Ili tufanikiwe katika mambo yoote tunatakiwa tujifunze kusikiliza neno la Mungu. Ndani ya somo hili tutajifunza namna ya kulipokea neno la Mungu ambalo ndani yake kuna maarifa na ufahamu yatokayo kutoka kwa Mungu.

 

Biblia inasema hivi “Mwanangu, kama ukiyakubali maneno yangu, Na kuyaweka akiba maagizo yangu; Hata ukatega sikio lako kusikia hekima, Ukauelekeza moyo wako upate kufahamu;Naam, ukiita busara, Na kupaza sauti yako upate ufahamu;”(Mithali 2:1-3)

 

Sikia tunaposikia kujifunza kuhusu habari za neno unabii fahamu tunazungumzia kuhusu habari ya neno la Mungu litokalo moja kwa moja kwenye ulimwengu wa roho. Neno hilo ndani yake linabeba ufahamu,maarifa nk.

 

Na amini umepata kujua malengo ya somo hili ni nini. Karibu tuanze kujifunza kuhusu somo hili.

Naamini umeelewa. Tuonane tena katika kona hii ya salamu za mwezi.

Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo:-

  1. App yetu ya huduma yenye jina “MWAKATWILA (HUSONEMU)” utaipata Play Store ambapo kuna masomo mengi sana hapo.
  2. Tovuti yetu ya www. mwakatwila. org
  3. YouTube – Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
  4. Facebook ingia katika hiyo tovuti (website) yetu utaona alama ya Facebook (f) “like” na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
  5. Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”
  6. DVDs au CDs
  7. VITABU. Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata VITABU, DVD & CD.
  8. Kwa njia ya REDIO: – Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
  • Rungwe FM 102. 5 Kila siku ya Jumapili saa tatu mpaka saa nne usiku.
  • Baraka FM 107. 7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
  • Bomba FM 104. 1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.

Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:- radio.mwakatwila.org

Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:- +255 754 849 924 au +255 756 715 222

Wako: Mwl Mr & Mrs Steven Mwakatwila.