Salamu – Aprili, 2024

Bwana Yesu Kristo asifiwe sana. Ninakukaribisha sana katika kona hii ya salamu za mwezi. Tunamshukuru Mungu ametupa mwezi huu.

Hebu tuanze kuzipokea salamu za mwezi. Kumbuka mwezi uliopita tulizipokea somo lenye kichwa.

JIFUNZE KUTAKA KARAMA AU KUOMBA MUNGU AKUPE KARAMA YA UNABII ILI UPATE KUFANIKIWA KIROHO WEWE NA WATU WENGINE (SEHEMU YA KWANZA)

Hebu tusogee mbele kidogo…

MUNGU ANATUTAKA TUSIKOSE KUJUA KUHUSU HABARI ZA KARAMA ZA ROHO.

Angalia mistari hii “Basi, ndugu zangu, kwa habari ya karama za roho, sitaki mkose kufahamu.” (1Kor 12:) NA “31 Takeni sana karama zilizo kuu. Hata hivyo nawaonyesha njia iliyo bora.” (1Kor 12:31).

Kwa mujibu wa mistari hii tunajifunza kuwa kuna habari ambazo Mungu anataka kumuona kila mtoto wa Mungu asikose kuzijua habari hizo.

Moja ya habari hizo ambazo Mungu anstaka kuona kila mtoto wa Mungu hakosi kuzijua habari hizo ni habari zinazo husu karama za roho.

Mungu anataka uzijue habari hizo na si kuzijua tu hizo karama za roho, Mungu pia anataka wewe uzitake karama hizo.

Sikia habari za karama za roho kiukweli ni shida sana kuzisikia habari hizo. Ukienda makanisani au kwenye semina nyingi ni mara chache sana kuzisikia habari au masomo ya karama za roho.

Moja ya somo au habari Mungu anataka tusikose kuzisikia au tujifunze ni somo hili la karama za roho. Kiukweli kuna masomo ambayo tunasikia sana…na watu wengi wanapenda kuzisikia,kama habari za kupata baraka za fedha, mali,vyeo, au kupiganiwa na maadui nk.

Watu wengi wanapoanza kuzisikia habari za karama za roho, watu wengi wanasita kuzisikia na kuanza kuzifuatilia.

Watu wengi wanaona kama ni mambo yanayowahusu watu furani tu. Sikia neno la Mungu linatutaka sisi wote kama ndugu tusikose kusikia habari za karama za roho. Maana yake hata wewe unatakiwa uzisikie na uzitake hizo karama za roho. Sikia kama Mungu anasema tusikose kuzijua habari hizi za karama za roho fahamu ni miongoni mwa habari muhimu mnoo.

MAANA YA NENO KARAMA

Neno karama maana yake ni zawadi. Unaposikia habari za karama roho maana yake ni zawadi ambazo roho ya mtu au watu wanapewa kwakusudi la kumsaidia au kuwasaidia.

Sikia Mungu alipotuumba ametuumba kwenye maeneo makuu matatu, tumeumbwa roho,nafsi,na mwili. Unaposikia kuhusu zawadi za roho fahamu zawadi hizo hupewa kwenye roho ya mtu.

Roho yako wewe inapopewa zawadi maana yake Mungu anakupa uwezo wa kiuungu rohoni mwako. Sikia kuna zawadi nyingi sana Mungu hutupa, moja ya zawadi ambazo Mungu anaweza kukupa ni hizo zawadi zinazo pelekwa moja kwa moja rohoni kwa watu.

Sikia, dhambi ilipofanywa pale bustanini Edeni kuna vitu viliharibika, moja ya vitu vilivyopotea ni uwezo wa rohoni mwa mtu.

Mungu alipotuumba alituumba kwa mfano na kwa sura ya Mungu. Biblia inasema hivi “Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.” (Mwanzo 1:26-27).

Kwa mujibu wa mistari hiyo utajifunza Mungu alipotuumba kwa mfano na kwa sura yake alikuwa amewekea nguvu au uwezo unaofanana na yeye alivyo.

Sikia Biblia inatufundisha kuwa kuwa Mungu ni Roho. “Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.” (Yohana 4:24).

Unaposikia Mungu alikuumba kwa mfano na kwa sura yake fahamu alikuumbia roho. Sasa sikia, unaposikia kuhusu habari za karama za roho fahamu zawadi hizo za roho zinahusu roho yako.

Sikia unaposikia habari za karama za roho maana yake ni uwingi..Biblia inaziita karama za roho. Biblia haisemi karama ya roho. Biblia inasema karama za roho. Kwa hiyo,zawadi hizo ni nyingi si chache. lazima ujue kuwa Mungu anataka awape watu (roho) zawadi nyingi tu.

Karama hizo za roho au zawadi hizo ambazo Mungu anaweza kuiipa roho yako ni hizi. Angalia mistari hii. “Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule;mwingine imani katika Roho yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja;na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha; lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye.” (1Kor 12:8-11)

Ukiisoma mistari hiyo utaziona hapo kuna karama za roho tisa.

1: Karama ya neno la Hekima

2: Karama ya neno la maarifa

3: Karama ya Imani

4: Karama za Kuponya

5: Karama ya matendo ya miujiza

6: Karama ya unabii

7: Karama ya kupambanua roho

8: Karama ya aina za lugha

9: Karama ya kutafsiri za lugha

Hizi ndiyo zawadi ambazo Mungu anaweza kukupa huko rohoni mwako. Sikia karama hizi za roho, Mungu anataka tusikose kujua kuhusu hizi karama za roho na tuzitake ili atupe.

Kwa leo tuishie hapa. Tuonane katika eneo hili la salamu za kila mwezi Mungu akubariki sana.

Naamini umeelewa. Tuonane tena katika kona hii ya salamu za mwezi.

Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo:-

  1. App yetu ya huduma yenye jina “MWAKATWILA (HUSONEMU)” utaipata Play Store ambapo kuna masomo mengi sana hapo.
  2. Tovuti yetu ya www. mwakatwila. org
  3. YouTube – Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
  4. Facebook ingia katika hiyo tovuti (website) yetu utaona alama ya Facebook (f) “like” na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
  5. Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”
  6. DVDs au CDs
  7. VITABU. Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata VITABU, DVD & CD.
  8. Kwa njia ya REDIO: – Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
  • Rungwe FM 102. 5 Kila siku ya Jumapili saa tatu mpaka saa nne usiku.
  • Baraka FM 107. 7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
  • Bomba FM 104. 1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.

Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:- radio.mwakatwila.org

Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:- +255 754 849 924 au +255 756 715 222

Wako: Mwl Mr & Mrs Steven Mwakatwila.