Salamu – Novemba, 2022

Bwana Yesu Kristo asifiwe sana.. Watoto wa Mungu ni siku nyingine. Tena nimewaletea salamu za mwezi..

Mwezi ulipopita tumekua na semina nyingi sana.. Tulikua na semina Manyoni,Itigi,Mvumi na Mpwapwa. Semina hizo tulifunga hema yaani tulifanyia nje..

Tumekuwa na semina nzuri sana sana.Nimekuletea salamu za mwezi wa kumi na moja. Kumbuka tunasalamu zenye kichwa

WEKA BIDII YA KUUSHUGHULIKIA MOYO AU NAFSI YAKO

Katika salamu za mwezi uliopita yaani wa kumi tuliendelea kuangalia madhara ya kuhifadhi uchungu moyoni..

Tulijifunza madhara ya pili ya kuhifadhi uchungu moyoni ni kukuharibia uso wako…

Hebu tuangalie madhara ya tatu ya kuhifadhi uchungu moyoni na kununa uso..

3: MADHARA YA TATU UCHUNGU UKIKAA MOYONI NA USO KUKUNJAMANA AU KUNUNA UNAPELEKEA WATU WENGINE WAWE NA UCHUNGU NA UTAWAONDOA KWAKO

Mungu hapendi unune au uso wako kukunjamana….Angalia alimwonya Kaini kutokana na jambo hili…”BWANA akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana?” (Mwanzo 4:6)

Uchungu uliojaa ghadhabu alio kuwa nao Kaini ulipelekea uso wake kukunjamana..

Fahamu, Mtu wa namna hii hupoteza uso wa asili aliopewa na Mungu na hujitengenezea sura ya kikatili ambayo Mungu haipendi

Sura ya namna hiyo inakukimbizia marafiki, ndugu na hata kuwajulisha watu udhaifu ulionao moyoni..

Unajua ukikunja uso hata watu wengine ulionao karibu hawawezi kuwa na furaha mioyoni mwao..

Angalia Biblia inasema hivi. “Maana umemfanya kuwa baraka za milele, Wamfurahisha kwa furaha ya uso wako.”(Zaburi21:6)

Mungu hutumia uso wake kuwatengenezea watu furaha.. fahamu. Akiunja uso wake watu hao hawataweza kuwa na furaha au amani kabisaa..

Hata wewe ni hivyo hivyo..ukiukunja uso wako unawatengenezea watu wengine huzuni… na watu hao watakukimbia tu.

Unapoukunja uso wako ndipo unapo watambulisha watu. wengine kuwa wewe unamatatizo.. na kwakuwa umenuna ni ngumu watu hao kukusaidia kwasababu watakuogopa..

Utajikuta upo peke yako.. Ukiwa na uso uliochangamka ni rahisi kuwavuta watu kwako na kukusaidia…

Mungu akusaidie katika eneo hili. Ili usikimbiwe na marafiki na ndugu nk

Ndugu naamini umenielewa Mungu akubariki sana tuonane tena mwezi ujao katika kona hii….

Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo:-

  1. App yetu ya huduma yenye jina “MWAKATWILA (HUSONEMU)” utaipata Play Store ambapo kuna masomo mengi sana hapo.
  2. Tovuti yetu ya www.mwakatwila.org
  3. YouTube – Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
  4. Facebook ingia katika hiyo tovuti (website) yetu utaona alama ya Facebook (f) “like” na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
  5. Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”
  6. DVDs au CDs
  7. VITABU. Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata VITABU, DVD & CD.
  8. Kwa njia ya REDIO: – Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
    • Rungwe FM 102.5 Kila siku ya Jumapili  saa tatu mpaka saa nne usiku.
    • Baraka FM 107.7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
    • Bomba FM 104.1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.
  9. Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:-  radio.mwakatwila.org

Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:-

+255 754 849 924 au +255 756 715 222

Wako

Mwl Mr & Mrs Steven Mwakatwila.