Salamu – Novemba, 2020

Bwana Yesu Kristo asifiwe. Ninakukaribisha tena katika eneo hili la salamu za mwezi. ili tupate kujifunza somo hili muhimu.

Hizi ni salamu za mwezi wa kumi na moja Kumbuka tunamfululizo wa salamu zenye kichwa.

MAMBO MUHIMU UNAYOTAKIWA UYAFANYE ILI UPATE WOKOVU (ENEO LA KUOKOLEWA KATIKA KIPINDI CHA MAJANGA ULIMWENGUNI)

JAMBO LA YA KUMI NA MOJA LEO OMBA MAARIFA

Ili Mungu atutoe kwenye tauni mbalimbali tunapomuomba,fahamu anaweza kukupa neno la maarifa ambalo ndani yake ndiyo limebeba uponyaji wako. Au taifa nk.

Neno maarifa maana yake ni uwezo apewayo mtu wa kutatua magumu aliyokutana nayo au kufanya mambo kwa ubora.

Mungu anajua kuwa mwanadamu anapokosa maarifa huangamia. Angalia mistari hii.

“Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; ”(HOSEA 4:6A)

Sasa sikia tauni inapokuja Mungu anaweza kukupatia maarifa kama taifa au mtu mmoja binafsi ya kukabiliana na janga hilo.

Ngoja nikupe mfano huu. Angalia mistari hii. “BWANA akatuma nyoka za moto kati ya watu, wakawauma, watu wengi wakafa. Watu wakamwendea Musa, wakasema, Tumefanya dhambi kwa sababu tumemnung’unikia Mungu, na wewe; utuombee kwa BWANA, atuondolee nyoka hawa. Basi Musa akawaombea watu. Bwana akamwambia Musa, Jifanyie nyoka ya shaba, ukaiweke juu ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa, aitazamapo ataishi. Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi.

“(Hesabu 21:6-9)

MUNGU ANAWEZA KUIBAKIZA TAUNI ILA AKAWAPA MAARIFA YA KUKABIRIANA NAYO

Mfano Mungu aliwapa maarifa hao ndugu walipokutana na tauni ya namna hiyo.. Mungu ni wa ajabu sana, fikiria kwanini asiwaondoe hao nyoka tu? Hao ndugu waliomba toba kabisa kwa Mungu.

Mungu hakuondoa nyoka,nyoka walikuwepo ila aliwapa hao ndugu wajibu wa nini kufanya. Aliwapa maarifa wafanye nini ili wakikutana na hiyo tauni watendenini.

Unajua unaweza ukawa unaomba Mungu ondoa hao nyoka Mungu akakuambia hao nyoka siondoi.

Ila akawafundisha watu NIDHAMU YA KUFANYA. Ataoa maarifa Ila ili kila aliyeumwa na nyoka ayafanye asipoyafanya atakufa.

JIFUNZE KUOMBEA VIONGOZI WA TAIFA NA WATU MAALUMU WAPOKEE MAARIFA

Sikiliza Mungu haweki maarifa kwa kila mtu, anachagua watu kwa rehema zake ndiyo anawawekea hayo maarifa katika kipindi hicho.

Angalia mfano huu

“Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana. Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule; mwingine imani katika Roho yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja;”(1Wakorintho 12:7-9).

SIkiliza mpendwa, ukiipitia hiyo mistari utaona Mungu hampi kila mtu neno la maarifa, anampa mtu mmoja na hampi kwa ajili yake anampa kwa kufaidiana.

Ngoja nikupe mfano mwingine. “BWANA akanena na Musa, na kumwambia, Angalia, nimemwita kwa jina lake Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila ya Yuda; nami nimemjaza roho ya Mungu, katika hekima, na maarifa, na ujuzi, na mambo ya kazi ya kila aina,ili abuni kazi za ustadi, kuwa fundi wa dhahabu, na wa fedha, na wa shaba, na kukata vito kwa kutiwa mahali, na kuchora miti, na kufanya kazi ya ustadi iwayo yote. Tena, tazama, nimemchagua, awe pamoja naye, huyo Oholiabu, mwana wa Ahisamaki, wa kabila ya Dani; nami nimetia hekima katika mioyo ya wote wenye moyo wa hekima, ili wapate kufanya vyote nilivyokuagiza; yaani, hema ya kukutania na sanduku la ushuhuda, na kiti cha rehema kilicho juu yake, na vyombo vyote vya Hema; na meza, na vyombo vyake, na kinara cha taa safi pamoja na vyombo vyake vyote, na madhabahu ya kufukizia uvumba; na madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na vyombo vyake vyote, na birika na tako lake; na mavazi yenye kufumwa kwa uzuri, na mavazi matakatifu ya Haruni kuhani, na mavazi ya wanawe, ili kutumika katika kazi ya ukuhani; na mafuta ya kutiwa, na uvumba wa manukato mazuri, kwa ajili ya mahali patakatifu; sawasawa na yote niliyokuagiza ndivyo watakavyofanya wao.”(Kutoka 31:1-11)

Mungu anasema nimemchagu huyo mtu ili ampatie maarifa. Sasa sikia nijambo dogo sana kwa Mungu kumpatia huyo mtu maarifa. Usifikiri maarifa hupewa kila mtu.

Mungu humpa neno la maarifa mtu mmoja ili huyo mtu awafundishe watu wengine. Ukiyakataa hayo maarifa usifikiri Mungu atakupa wewe. Najua watu wengi hawajui kuwa KUNA WATU WAMEBEBA MAARIFA MENGI KWA AJILI YAO LAKINI HAWATAKI KUWASIKILIZA KWASABABU ZAO ZA KIJINGA.

Utasikia huyu hasali kwetu, huyu, amebatizwa maji ya mfumo furani nk. Kuna watu nakwambia ndiyo wamebeba ndani yao maarifa wa ajili ya ndoa yako,maarifa kwa ajili ya uchumi wako. Usipowasikiliza utakwama tu.

Katika kipindi cha majanga ya namna hii. Jifunze kuwaombea viongozi wa nchi yetu Mungu awajaze maarifa nini wafanye katika kipindi hiki, omba maarifa kwa Mungu ya wewe mwenyewe ufanye nini katika kipindi hiki.

SEHEMU TATU ZINAZO WEZA KUACHILIA MAARIFA

Unajua kuna maarifa ya kutoka kwa wanadamu na kutoka kwa Mungu na kutoka kwa shetani.

Katika kipindi kama hicho lazima uwe makini kupokea hayo maarifa. Mfano wakati wa tauni ya corona kulikua na maarifa mengi, mfano

Kuna mataifa yalifungia watu ndani, nhalo lazima ujiulize nani kasema watu wajifungie ndani? Ili wasipate corona? Maarifa hayo yametoka kwa nani? Mtu, Mungu au shetani? Kwasababu Mungu aweka mataifa, kila taifa linaweza kupewa maarifa yake.

Unajua kuna maarifa mengi unaweza kuyasikia, wakati wa corona 19 ttulisikia tuvae barakoa,tunawe mikono nk. Lakini swali maarifa hayo yametoka wapi? ni Mungu ni watu au ni shetani?

Kuna suala la dawa ipi itumike katika kuponya na hili la chanjo. Kanisa lazima kuomba maarifa ya kutoka kwa Mungu katika mambo haya.

UCHUMI UTAPAA KAMA MAARIFA YATALETWA NCHINI MWETU

Tuombe Ili Mungu aachilie neno lake la maarifa iwe kwa wataalamu wetu humu ndani au huko ulimwenguni wajue dawa na chanjo.

Ngoja nikupe mfano.umefikiri nini kuhusu dawa ya kutibu tauni itokee nchini mwetu? Si tutaendelea sana, uchumi utakua mkubwa mno.

Angalia mfano wa kule Misri. Mungu alipoleta njaa, nchi ile ilipewa mtu maalumu aliyeyajua maarifa ya nini wafanye katika kipindi cha njaa kali kutokea duniani.

Yusufu mtumishi wa Mungu alipewa maarifa, Falao mkuu wa nchi alipokea hayo maarifa kutoka kwa Yusufu, Yusufu alipokea kutoka kwa Mungu. Angalia uchumi wa Misri ulipaa ghafla. Haya ndiyo yakuliombea taifa hili

Watumishi wa Mungu tusisite kuongea na viongozi wa serekali tunapopokea maarifa kutoka kwa Mungu. Pia viongozi wa serekali kipindi kama hicho wanahitaji sana kupokea maarifa kutoka kwa watumishi wa Mungu pia.

Anza kuomba maarifa usishangae ukapata hata muongozo wa nini ufanye katika kipindi hiki katika eneo la uchumi wako, Ngoja nikupe mfano matatizo yanapotokea wakati furani ndiyo fulsa yakiuchumi itafunguliwa kwako.

Hata huku ndani ya kanisa. Majanga kama haya yakitokea Mungu anaweza kukupa mchungaji maarifa, mfano hivi hofu hii iliyoikumba ulimwengu kanisa lmeiona katika eneo la kuujenga ufalme wa Mungu? Unafikiri nini juu ya hofu hii omba maarifa ya namna ya kuujenga ufalme wa Mungu. kwa kuitumia hofu hii. Ni fulsa kwa ufalme.

Mungu akabariki

Mungu akubariki sana. Tuonane tena katika kona hii mwezi ujao.Naamini umenielewa sana.Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo:-

  1. App yetu ya huduma yenye jina  “MWAKATWILA (HUSONEMU)” utaipata Play Store ambapo kuna masomo mengi sana hapo.
  2. Tovuti yetu ya www.mwakatwila.org
  3. YouTube – Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
  4. Facebook ingia katika hiyo tovuti (website) yetu utaona alama ya Facebook (f) “like” na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
  5. Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”
  6. DVDs au CDs
  7. VITABU. Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata VITABU, DVD & CD.
  8. Kwa njia ya REDIO:- Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
    • Rungwe FM 102.5 Kila siku ya Jumapili  saa tatu mpaka saa nne usiku.
    • Baraka FM 107.7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
    • Bomba FM 104.1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.
  9. Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:-  radio.mwakatwila.org

Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:-

+255 754 849 924 au +255 756 715 222

Wako

Mwl Mr & Mrs Steven Mwakatwila.